06/08/2026
Kazi Yangu Ikiisha
[1]
Kazi yangu ikiisha, nami nikiondoka,
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi nifikapo ng'amboni,
Atakuwa wa kwanza kunilaki.
[refrain]
nitamjua, nitamjua nikimwona uso kwa uso,
Nitamjua,nitamjua kwa alama za misumari
[2]
Furaha nitapata nikiona makao
Bwana aliotuandalia
Nitamsifu Mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni
[3]
Naowaliokufa katika Bwana Yesu
nitawaona tena huko juu
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
[4]
Milangoni mwa mji Bwana atanipisha
Pasipo machozi wala huzuni
Nitaimba wimbo wa milele; lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza