22/06/2026
Natumai umzima wa afia karibu kwa neno
2 Timothy 1:7
"Maana Mungu hakutupa roho ya woga; bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi."
mambo ma ene yakujifuza
1. Siyo roho ya woga
Woga hutuzuia kutimiza mapenzi ya Mungu.
Mungu hataki watoto wake waishi kwa hofu, mashaka, au kukata tamaa.
2. Roho ya nguvu
Roho Mtakatifu hutupatia uwezo wa kushinda majaribu, mateso, na changamoto za maisha.
Nguvu hii si ya kibinadamu bali ni ya Mungu.
3. Roho ya upendo
Upendo wa Mungu humiminwa mioyoni mwetu kupitia Roho Mtakatifu.
Hutuwezesha kuwapenda Mungu na watu wengine hata katika mazingira magumu.
4. Moyo wa kiasi (akili timamu)
Roho Mtakatifu hutupa hekima, nidhamu, na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
Hutusaidia kutenda kwa busara badala ya kuongozwa na hofu au hisia.
Muumini aliyejazwa na Roho Mtakatifu hapaswi kutawaliwa na woga. Badala yake, anapaswa kuishi kwa nguvu za Mungu, upendo wa Kristo, na akili timamu. Wakati hofu inapokuja, kumbuka kwamba Mungu tayari amekupa Roho wa ushindi.
Kauli Kuu
"Woga hutazama ukubwa wa tatizo, lakini Roho Mtakatifu hutufunulia ukuu wa Mungu."