03/02/2026
Seif al-Islam Gaddafi, mwana wa mtawala wa zamani wa Libya, amefariki dunia, jamaa zake wameripoti Jumanne bila kutoa maelezo kuhusu sababu au mazingira ya kifo chake. Mshauri wake, Abdallah Othman Abdurrahim, alithibitisha taarifa hizo kupitia chapisho la mitandao ya kijamii, bila kueleza undani zaidi. “Seif al-Islam amefariki,” alisema binamu yake, Hamid Gaddafi, akiieleza televisheni ya Libya, al-Ahrar, na kuongeza kuwa familia haina taarifa zaidi kwa sasa. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa amefariki katika mji wa Zintan, kaskazini magharibi mwa Libya, ingawa mahali alipoishi kwa miaka ya hivi karibuni hapakuwa wazi. Seif al-Islam, mwenye umri wa miaka 53, alikuwa akitazamwa k**a mrithi wa baba yake.