30/09/2020
BIDHAA ZENYE KEMIKALI Vs MATUNDA HALISI
Katika urembo kumekuwa na matumizi makubwa ya bidhaa za urembo zinazotengenezwa kwa kemikali ambazo sio salama katika afya ya mtumiaji.
Mtu kutumia sabuni au mafuta yaliyo tengenezwa kwa tunda au mboga mboga pamoja na kemikali na kuacha kula tunda au mboga mboga halisi bila kujua kuwa kemikali zilizopo katika bidhaa anayotumia zina madhara katika afya yake.
Aliyewai kuwa mmoja kati ya watumiaji wa bidhaa za urembo zenye kemikali ndugu Tea Skrjanec aliwai kusema " Nilipoanza safari ya kula matunda na mboga mboga nilijikuta naachana na vitu vyote vya bandia katika maisha yangu.
Niligundua uzuri hauletwi na bidhaa za urembo bali afya bora. Makampuni makubwa ya bidhaa za urembo yanatuhaminisha kununua bidhaa zao kwa kigezo tutapata matokeo mazuri tutakapo tumia bidhaa zao, ukweli ni kwamba bidhaa hizo zina kemikali ambazo ni sumu ambazo huwezi kuziona nje ya mwili. Matumizi ya bidhaa hizi za kemikali mwishowe husababisha mwili kuwa na sumu kupita kiasi, na sumu hizi zinahusishwa na kusababisha magonjwa k**a Saratani(kansa),mimba kuharibika,mzio(allergy), uharibifu wa mfumo wa kinga,ngozi kuwa kavu,utasa na uharibifu wa manii.
Katika maisha yangu ya ujana nilikuwa na mawazo ya kuwekeza pesa zangu katika mwili wangu k**a kununua mapambo,vipodozi,nguo,viatu na vitu vingine vya urembo.
Sikujua k**a vitu hivi vilikuwa na sumu ambayo mwisho wa siku zitaniletea madhara."